NEMANJA MATIC NA MOUSSA SISSOKO WATAJWA KUMRITHI POGBA JUVENTUS

Kiungo wa Chelsea Nemanja Matic na kiungo wa Newcastle Moussa Sissoko wanatajwa kuwaniwa na Juventus ambao ni mabingwa wa Italia.



Sakata la Paul Pogba kuihama klabu hiyo ya Juventus liko katika hatua ya mwisho na tayari Juventus wameona ni bora kujiandaa kuziba pengo la nyota huyo huku Matic na Sissoko wakitajwa sana kuwa wachezaji watakaosajiliwa.

Pia katika orodha iliyosambaa katika vyombo vingi vya habari imewataja pia Andre Gomes wa Valencia, Axel Witsel wa Zenit na Marcelo Brozovic wa Inter Milan.



No comments

Powered by Blogger.