PENATI ZAIBEBA GENK YA SAMATTA KUSONGA MBELE KATIKA EUROPA LEAGUE
Klabu ya Genk ya Ubelgiji ambayo ni klabu anayochezea nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta imesonga mbele katika michuano ya Europa League baada ya kushinda kwa penati 4-2 katika mchezo wa pili hatua ya pili ya mtoano katika michuano hiyo.
Genk ambayo ilishinda mechi ya awali nyumbani bao 2-0 ilijikuta ikishindwa kulinda mabao yao na kuruhusu kufungwa bao 2-0 pia na Buducnost ya Montenegro hali iliyopelekea kuongezwa dakika 30 badae mikwaju ya penati ambayo Genk walishinda 4-2.
Katika mechi hiyo ambayo Samatta alicheza dakika zote 90 Pongezi nyingi ziwaendee Genk baada ya kucheza pungufu tangu dakika ya 75 baada ya Bennard Kumordzi kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Genk sasa watacheza hatua ya mwisho ya mtoano katika michuano hiyo dhidi ya Cork City ya Jamhuri ya Ireland na wakifanikiwa kupita hapo basi wataingia katika makundi.

No comments