ICC : MANCHESTER UNITED DHIDI YA BORUSSIA DORTMUND LEO MCHANA

Michuano ya International Champions Cup (ICC) kanda ya China inaanza leo kwa mechi kali baina ya Manchester City ya England na Borussia Dortmund ya Ujerumani.


Mechi hiyo itapigwa muda wa saa 9 alasiri kwa saa za hapa nyumbani na utakua mchezo wa pili kwa kikosi cha kocha Jose Mourinho aliyechukua jukumu kuifundisha klabu hiyo akirithi mikoba ya Luis Van Gaal.

Michuano hiyo hufanyika katika kanda 3 (Marekani, Australia na China) wakati huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya kila mwaka.

Katika kanda ya China zipo timu 3 ambazo ni Manchester United,Manchester City na Borussia Dortmund na timu yenye pointi nyingi katika michezo hiyo miwili kwa kila timu ndiyo itakua bingwa.

No comments

Powered by Blogger.