LEICESTER CITY YAVUNJA REKODI KUMSAJILI AHMED MUSSA

Mabingwa wa ligi kuu nchini England Leicester City wametangaza rasmi kumsajili mshambuliaji wa Nigeria na klabu ya CSKA Moscow Ahmed Musa kwa Dau lililovunja rekodi ya usajili wa klabu hiyo paundi milioni 16.




Musa mwenye miaka 23  ni tegemeo katika kikosi cha Super Eagles na akiwa na kukosi cha CSKA msimu  uliopita aliweza kufunga magoli 13 katika Mechi 30 za Ligi kuu nchini Russia na magoli 18 katika mashindano yote.

Huyu ni Mchezaji wa 4 kusainiwa na Leicester City katika kipindi hiki cha usajili baada ya kukamilisha usajili wa Nampalys Mendy, Ron-Robert Zieler na Luis Hernandez.


2 comments:

Powered by Blogger.