MARTIAL ASIPOACHA UTOTO KAMWE HATOTENGENEZA ASALI
Anthony Martial.. Kinda ghali zaidi duniani anayekipiga katika klabu ya Manchester United amekuwa akipata wakati mgumu sana kwa sasa katika kikosi cha timu yake ya taifa ya Ufaransa. Akiwa ameingia kama mchezaji wa akiba na kuanza game nyingine kipindi kimoja tu ameshindwa kabisa kumshawishi kocha wake hadi kupelekea Olivier Giroud kuaminiwa zaidi yake licha ya makosa mengi aliyoyafanya kwenye mechi ya nusu fainali.
Kiungo wa zamani wa United Paul Scholes amekuwa akimtuhumu sana mchezaji huyu, haamini kuwa thamani yake na kile anachokifanya hakuna mwingine pale klabuni angeeza kukifanya.. Kwake yeye thamani ya makinda pale klabuni ni kubwa kuliko wanaonunuliwa kwa pesa kubwa. Yeye anaamini kama wakipewa nafasi ya kutosha watoto waliokulia klabuni, wanaoelewa vizuri utamaduni wa Man UTD wanaweza fanya makubwa kuliko Martial.
Na kuongeza kuwa anaonekana anafanya makubwa kwa sababu tu hali ya timu kwa sasa si nzuri, ila kwa namna moja au nyingine anaigharimu sana timu kwa makosa yake madogo madogo anayoyafanya yakiwemo maamuzi ya kipumbavu yasiyokomaa.
Unaweza jiuliza, hivi kwa nini Ufaransa haaminiwi tena?.. Jibu ni rahisi tu kuwa utoto wake ulikaribia kuigharimu timu yake ya taifa. Uwezo wake wa kuddrible ni mkubwa mno lakini ni mwepesi wa kupoteza mipira halafu hakabi.. Anapenda mno kujiangusha, na hata akifanikiwa kuingia ndani ya box tegemea maamuzi ambayo hayajakomaa.
Nafasi yake chini ya kocha mpya wa klabu yake ipo shakani kwa sababu Mourinho hapendi wachezaji wa aina yake. Unaeza kuwa bora kwako mwenyewe na kwa mashabiki ila si kwake yeye. Anaamini kuwa kama huezi kukaba basi huwezi isaidia timu kupata matokeo mazuri. Kama unabisha muulize Juan Mata kilichomtokea wakati yupo Chelsea. Anaweza mpa nafasi mbili tatu lakini atakapozingua unaweza kuta Memphis Depay anamrithi eneo lile la pembeni, au Ashley Young kuwa na namba ya kudumu.
"Maturity" inahitajika kwa kiasi kikubwa kwa kinda huyu ili aendelee hata kuinusa ile tuzo ya kikubwa, sivyo ataendelea kuwa mshuhudiaji tu na hata jina lake linaweza potea mapema zaidi ya afikiriavyo lasivyo INABIDI AACHE UTOTO ILI AWEZE TENGENEZA ASALI.
Imeandaliwa na Sylvaddict : Member WST

Makala imeongea jambo la maana kuhusu Martial lakini kuna machache ya kukumbuka;
ReplyDelete1. Utoto wa Martial utaondoka/kupungua kadri anavyokua na kuzoea mazingira ya EPL
2. Umri aliopo ni umri wa mchezaji kujiachia, kujaribu, na kuwa huru uwanjani sababu ndo kwanza yuko hatua za mwanzo za uchezaji wake!
3. Martial vs Giroud timu ya taifa ya Ufaransa? Hii si kweli, Giroud anamuweka benchi Andre Pierre Gignac, japo Martial anaweza kucheza kama namba 9, ila Ufaransa nafasi yake anagombea na wachezaji wengine wa pembeni, sidhani kama ni sahihi kusema Giroud anaaminiwa Ufaransa zaidi ya Martial, hawachezi nafasi moja!
Martial ni mchezaji mzuri sana, kwa umri wake bado anavumilika na kufundishika, naamini kadri anavyokua basi hata maamuzi yake uwanjani yatakuwa ya kikubwa zaidi