ABDALLAH HAMIS: LULU YA TANZANIA ILIYOJIFICHA NA KUNG'AA NJE YA MIPAKA YA NCHI.. 

Kijana kutoka Tarime anajulikana kwa jina la ABDALAH HAMIS akicheza nafasi ya kiungo mkabaji, huku akiwa na umri wa miaka 23 tu ni mmoja kati ya vijana wachache walioweza kuvuka mipaka na moja kwa moja kuanza kuichezea klabu ya Muhoroni inayoshiriki ligi kuu nchini Kenya.


Abdallah maarufu kama DULLA alianzia soka lake nyumbani kwao Tarime akizichezea timu za Tarime United na baadae Tarime Warriors, kabla ya kutimkia Stand Unadae Chama la Wana ya mjini Shinyanga na kuisaidia kupanda daraja hadi ligi kuu..

Baada ya hapo Dullah aliingia nchini Kenya na kuanza kuchezea kikosi cha vijana cha Muhoroni kabla ya kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha wakubwa.

Nilipofanya naye mahojiano wiki iliyopita Dullah aliniambia kwa furaha,

"Nafurahi sana kupata nafasi katika kikosi cha kwanza, mwalimu ananiamini na kunifanya nijiamini, naamini ipo siku nitachezea timu yangu ya taifa" alisema.

Moja kati ya nafasi adhimu katika mpira wa kisasa ni nafasi ya kiungo mkabaji anayoichezea Dullah.

Ninapoona mchezaji anayechezea klabu yoyote ile anapata nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza katika nafasi ya kiungo mkabaji huwa naamini kuwa ana kitu fulani cha ziada.

Kazi ya kulinda walinzi, "ku-block" mashambulizi ya maadui, kuanzisha mashambulizi nk, hii unahitaji mtu makini, imara kimwili na kiakili, mwenye mtazamo wa mbali na mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu.

ABDALLAH HAMIS licha ya umri lakini kimo chake pia vinamfanya kuwa lulu iliyofichika na kung'aa nje ya mipaka.

Tayari kuna taarifa kuwa klabu ya Sofapaka kutoka kule kule nchini Kenya inahitaji huduma yake ingawa mwenyewe hakuwa tayari kulizungumzia hilo lakini naamini siku zote muda utaongea..

Huyo ndiye ABDALLAH HAMIS lulu iliyofichika inayong'aa nje ya mipaka...


Imeandikwa na:

Martin Maranja Masese
Mwananchi wa kawaida

No comments

Powered by Blogger.