BAADA YA KUMKOSA ZIELINSKI LIVERPOOL WAHAMIA KWA KIUNGO WA NEWCASTLE GIORGINIO WIJNALDUM

Liverpool wanaendelea na mbio zao za kuimarisha kikosi chao kwa kufanya usajili katika idara karibia zote muhimu tayari kwaajili ya msimu ujao.


Baada ya kumkosa kiungo wa Udinese Piotr Zielenski ambaye ameamua kujiunga na AC Milan, klabu hiyo sasa imehamishia nguvu zake sasa katika kutaka kumsajili kiungo wa Newcastle na timu ya taifa ya Uholanzi Giorginio Wijnalnzi.

Japokua Newcastle hawako tayari kumwachia lakini taarifa zinasema kwamba Mchezaji huyo atatoka Newcastle ikiwa tu ada ya uhamisho wa paundi milioni 25 itafikiwa na Liverpool.

Newcastle United walitumia kiasi cha paundi milioni 14.5 kumsajili mchezaji huyo toka PSV Eindhoven mwaka mmoja uliopita.

Wijnaldum ambaye alifunga mabao 11 msimu uliopita anawaniwa pia na Tottenham


No comments

Powered by Blogger.