MAN UNITED YAONGEZA MDHAMINI MWINGINE NI WA 15

Manchester United imeongeza idadi ya wadhamini wake kwa kusaini mkataba na kampuni ya Virgin Money inayojihusisha na maswala ya fedha.


Mmiliki wa Virgin Money akiwa na Jezi ya Man United
Virgin Money inayomilikiwa na Richard Branson inakua kampuni ya 15 kuidhamini klabu hiyo katika maswala ya fedha ngazi ya "Retail" ikiwa ni kusimamia biashara mbalimbali zinazohusu klabu katika nchi zaidi ya 70 na imesaini mkataba wa miaka mitano.

Idadi ya wadhamini ambao Manchester United inao mpaka sasa ni mara mbili ya wadhamini wa klabu nyingine yoyote katika ligi kuu ya England



No comments

Powered by Blogger.