TUZO YA MCHEZAJI BORA BARANI ULAYA, 7 WATOKA LALIGA,EPL PATUPU

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetoa orodha ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya mwanasoka bora barani Ulaya kwa mwaka huu.




Wachezaji hawa 10 watapigiwa Kura toka kwa Wanahabari maalum toka Nchi 55 Wanachama wa UEFA hapo Agosti 5 ili kubakiza watatu  Bora ambapo mmoja wao ataibuka kuwa Mshindi na kutangazwa Agosti 25 wakati wa Droo ya kupanga Makundi ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya huko Monaco Ufaransa.

Macho na masikio ya wengi yatakua kwa wakali wawili Ronaldo na Messi lakini Luis Suarez anatarajiwa pia kuleta upinzani.

Wachezaji 7 wanatoka katika ligi kuu nchini Spain wakati wawili wanatoka Bundesliga na mmoja Ligi kuu ya Italia huku kukiwa hakuna mchezaji yeyote toka katika ligi kuu ya England.

Lionel Messi anashikilia tuzo hiyo kwa sasa baada ya kuitwaa mwaka jana na kama atatwaa tena mwaka huu basi atakua ametwaa kwa mara ya tatu.

Ukiacha Messi ambaye aliwahi kushinda tuzo hiyo pia mwaka 2011 wengine walioshinda tuzo hiyo ni Andrés Iniesta (2012), Franck Ribéry (2013) and Cristiano Ronaldo (2014).

ORODHA YA WACHEZAJI 10 WANAOWANIA TUZO HIYO

  • Gareth Bale (Real Madrid & Wales)
  • Gianluigi Buffon (Juventus & Italy) 
  • Antoine Griezmann (Atlético Madrid & France)
  • Toni Kroos (Real Madrid & Germany)
  • Lionel Messi (Barcelona & Argentina)
  • Thomas Müller (Bayern München & Germany)
  • Manuel Neuer (Bayern München & Germany)
  • Pepe (Real Madrid & Portugal)
  • Cristiano Ronaldo (Real Madrid & Portugal)
  • Luis Suárez (Barcelona & Uruguay)



No comments

Powered by Blogger.