TUZO ZA MSIMU WA 2015-16 TUMEZIONA LAKINI HAPA HAMJATENDA HAKI.

Sherehe za ugawaji wa tuzo kwa wachezaji,makocha na timu zimefanyika usiku wa tarehe 17 Julai. Kiukweli zimegawiwa kwa haki na wote waliofanikiwa kushinda hizo zawadi walistahili kutokana na kazi waliyoifanya msimu ulioisha.


Pamoja na sherehe hizo kufanyika imeonekana ni wazi hamna muunganiko au mpangilio yakinifu katika tuzo hizo. Katika tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuna wazawa pekee ina maana wageni hawakushiriki katika ligi!!? Au wageni hawakuonyesha uwezo ambao wazawa waliuonyesha!? Hakuna haki katika hili kuwagawa wachezaji si vizuri,kwani hawakucheza pamoja!? Basi tujifunze hata nchi za ng'ambo zilizoendelea hasa pale wanapokuwa na tuzo ya mchezaji bora wa ligi,mchezaji bora mzawa na mchezaji bora wa kigeni.

Pia tumeona Ajib ameshinda tuzo ya goli bora la msimu akiwa amempiku Tambwe wa Yanga katika list hiyo imeonekana Ajib ameingiza magoli mawili. Sasa ni goli lipi lililompa zawadi hiyo!? Hakuna anayejali katika hilo mambo haya si ya kufanya kwa mazoea.

Ni wapi uliona mchezaji au mtu yoyote anaposhinda tuzo hapati nafasi ya kushukuru!? Ndivyo ilivyo tokea. Kutoa shukrani ni jambo jema hasa kwa watu waliompigia kura kwa kuheshimu na kuona mchango wake katika timu aliyokuwa na ligi kwa ujumla.

Kocha wa Yanga Hans Plujim alipoona kipaza sauti tu akakisogelea na kuanza kutoa shukrani lakini hakuna aliyempa nafasi hiyo. Hata Juma Abdul ni baada ya kuitwa kwa mara ya pili ndio aliongea.

Sasa tugeukie wachezaji na wahusika wengine wa hizo tuzo. Wachezaji ni soko ambalo linatembea lakini kwa tuzo zile ni hakuna mchezaji aliyejali muonekano wake. Ni heshima na busara kuwa katika hali nadhifu katika mkusanyiko ule wa watu wa aina mbalimbali hasa kinyadhifa na umri. Hatuwaoni wakina Messi wanavyopendeza pale hakuna anayevaa kama anaenda kwenye disco au shoo ya muziki. Katika hilo tubadilike.

Hatuwezi kusema ule ndo usiku wa kwanza wa sherehe hizo kufanyika. Mara nyingi kumekuwa na makosa ya wazi kabisa ambayo yangeweza kurekebishika kabla muda au siku husika kufika. Hali hiyo inaonyesha hakuna anayesimamia majukumu yake kwa ufasaha yani kila mtu atajua mwenyewe. Hatwendi hivyo. Hapo hamjatutendea haki.

No comments

Powered by Blogger.