WEST HAM WAMSAJILI WINGA WA ALGERIA TOKA VALENCIA

Klabu ya West Ham United ya England imekamilisha usajili wa winga wa kimataifa wa Algeria Sofiane Feghouli toka Valencia ya Spain.


Feghouli anajiunga na West Ham  kwa mkataba wa miaka mitatu kuanzia Julai Mosi kwa kiasi ambacho hakijawekwa wazi.

Feghouli alikamilisha vipimo vya afya na kukaubaliana masharti ya mkataba siku ya Jumatatu

Kiasili Feghouli ni Mfaransa kwani alizaliwa Paris lakini amechukua uraia wa Algeria kwa baba yake alijiunga na Valencia mwaka 2010 akitokea Grenoble ya Ufaransa ameifungia Valencia magoli 42 katika michezo 243.



No comments

Powered by Blogger.