HAKUNA TENA UMITASHUMTA WALA UMISSETA MPAKA TUPATE MADAWATI.

Serikali imetoa tamko la kuairisha mashindano ya umoja wa michezo na Taaluma kwa shule za Msingi na Sekondari Tanzania (Umitashumta na Umisseta) ili kupisha zoezi la kumaliza upungufu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari hadi hapo yatakapotangazwa tena.



Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Waziri wa ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene amesema mashindano hayo yameahirishwa ili kupisha zoezi la kumaliza upungufu wa madawati kwenye shule za msingi na sekondari kwani wadau muhimu wa mashindano hayo wote wanahitajika katika kumaliza tatizo hilo.

No comments

Powered by Blogger.