SINGIDA UNITED YATWAA USHINDI WA TATU SPORTPESA SUPER CUP


Timu ya Soka ya Singida United kutoka mkoani Singida imeibuka washindi wa tatu katika michuano ya SportPesa Super Cup mechi iliyopigwa mchana huu dhidi ya KK Homeboys ya Kenya.

Singida United imeibuka na ushindi wa penati 4-1 baada ya kumaliza dakika 90 mechi Ikiwa ni sare ya bao 1-1.

Dakika ya tano tu ya mchezo Singida walikubali kufungwa bao la kwanza ambalo lilidumu mpaka Mapumziko licha ya juhudi kubwa za kutaka kusawazisha kukwama.

Kipindi cha Pili Danny Lyanga aliisawazishia Singida United bao dakika ya 61 na kufanya mchezo huo kumalizika Kwa sare ya bao 1-1 hivyo mikwaju ya penati kuamuru bingwa wa mchezo huo.

Singida United walipata penati zao zote nne walizopiga kupitia Kwa Deus Kaseke, Miraji Adamu, Shafiq Batambuze na Danny Lyanga huku KK Homeboys wakipata penati moja pekee huku penati mbili wakikosa moja ikipaa  juu na nyingine ikidakwa na kipa wa Singida United Manyika Jr.

Deus Kaseke aliibuka Mchezaji bora wa mechi hiyo akipata zawadi ya mpira pamoja na hundi ya dola 500 za Marekani.

No comments

Powered by Blogger.