SIMBA YACHEMKA SAFARI YA KUCHEZA NA EVERTON, YAFUNGWA NA GOR MAHIA
Ndoto za Mabingwa wa Soka Tanzania bara wekundu wa Msimbazi Simba kupata nafasi ya kwenda England kucheza dhidi ya Everton imeyeyuka baada ya kufungwa bao 2-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.
Simba walikuwa wakicheza kwa mara ya kwanza fainali yao ya SportPesa Super Cup dhidi ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo ambao pia ni mabingwa wa Kenya klabu Gor Mahia
Mabao ya Gor Mahia yamefungwa na washangiliaji wake Medie Kagere ambaye amekuwa pia Mfungaji bora wa michuano hiyo akifikisha mabao manne ambayo yamempa tuzo ya Mfungaji bora na bao la pili likifungwa na Jacques Tuyisenge kipindi cha pili.
Matokeo hayo yanawafanya Gor Mahia kupata nafasi ya kusafiri mpaka England baadae mwezi ujao kucheza mechi dhidi ya Everton.
Pengine kukosekana kwa wachezaji takribani 6 wa kikosi cha kwanza ndiyo moja ya sababu ya Simba kushindwa kufurukuta mbele ya mabingwa hao wa Kenya ambao wamekuwa na wachezaji wao wote huku wakitokea katika ligi kuu ya Kenya ambayo inaendelea.

no team like yanga in tanzania
ReplyDelete