STAND UNITED YAMSAJILI YUSUPH MPILIPILI TOKA TOTO AFRICANS YA MWANZA

Klabu ya Stand United ya Mjini Shinyanga imeendelea na maandalizi yake ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa kukiimarisha kikosi chake.




Tayari Stand United imekamilisha usajili wa beki wa Zamani wa African Lyon ya Dar Es Salaam na Toto Africans ya jijini Mwanza Yusuph Mpilipili.

Tayari Beki huyo mwenye kipaji cha kucheza kama beki wa kati na beki wa pembeni kulia ameshasaini kandarasi ya  miaka miwili kuichezea Stand United ambayo inadhaminiiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA na atajiunga na kikosi cha Stand siku chache zijazo katika maandalizi ya msimu mpya.

Mbali na beki huyo Stand United inaendelea na mipango yake kabambe ya kuiimarisha kikosi chake ili kufanya vizuri katika michezo yake ya ligi kuu ya Vodacom na ile ya Kombe la Shirikisho Tanzania (Azam Federations Cup)

Imetolewa na 
ALEXANDER SANGA 
MKURUGENZI WA HABARI NA MAWASILIANO 
STAND UNITED COMPANY LIMITED 
0715052491

No comments

Powered by Blogger.