EURO 2016 : SPAIN NA ITALIA ZATINGA HATUA YA MTOANO, CROATIA NA CZECH SARE

Mabingwa watetezi wa michuano ya Euro 2016 Spain na Italia wametinga hatua ya mtoano baada ya kuibuka na ushindi katika mechi zao za jana.



Katika kundi D Spain iliitwanga Uturuki kwa bao 3-0 ikiwa rekodi ya kuwa timu ya kwanza kupata ushindi wa zaidi ya goli 3 katika michuano ya mwaka huu tangu ilipoanza Juni 10.

Magoli ya Spain ambayo sasa imefikisha pointi 6 yalifungwa na Alvaro Morata aliyefunga magoli mawili na Nolito aliyefunga goli moja.

Croatia yenyewe ililazimishwa sare ya bao 2-2 na Jamhuri ya Czech, Croatia ikipata magoli yake kupitia kwa Ivan Perisic na Ivan Rakitic wakati Czech walipata magoli yao kupitia kwa Milan Skoda na Tomas Necid.

Mchezo huo pengine unaweza kuwafanya Croatia wakatolewa mashindanoni baada ya mashabiki wake kuleta fujo na kutupa mafataki uwanjani wakipinga mwamuzi Mark Clattenburg kuwapa Zcech penati dakika za lala salama.

Katika mechi moja tu ya kundi E hiyo jana Italia ilitinga hatua ya mtoano baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sweden bao pekee la mshambuliaji Eder.

No comments

Powered by Blogger.