PACHA WA DONALD NGOMA AWASILI DAR KUJIUNGA NA YANGA
Baada ya mafanikio makubwa yaliyoletwa na mshambuliaji wa zamani wa Platnum Stars ya Zimbabwe Donald Ngoma mabingwa wa Tanzania bara Yanga wameamua kumleta pacha wake katika ushambuliaji wakati akiwa katika timu hiyo ya Zimbabwe.
Anaitwa Obrey Chirwa raia wa Zambia akicheza kama kiungo mshambuliaji tayari amewasili Dar es Salaam kukamilisha uhamisho wake na kusaini mkataba wa kuwachezea mabingwa hao wa bara ambao wako Algeria hivi sasa kwaajili ya mechi ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Usajili wa Mchezaji huyo ambaye pia huweza kushambulia akitokea upande wa kulia ni pendekezo la Donald Ngoma ambaye anaamini ataisaidia Yanga.
Taarifa zinasema mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kucheza katika klabu hiyo ya Jangwani.

No comments