SIMBA YAMSAJILI MCHEZAJI MWINGINE TOKA MTIBWA SUGAR
Wekundu wa Msimbazi Simba wameendelea na mawindo yao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara na michuano ya kombe la Shirikisho Tanzania kwa kumsajili mchezaji mwingine toka Mtibwa Sugar.
Baada ya kukamilisha usajili wa Muzamil Yasin kutoka Mtibwa Sugar Simba wamerudi tena kusajili mchezaji mwingine kwa wakata miwa hao na safari hii imemsajili Mohammed Ibrahim kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekwa wazi lakini kukiwa na kipengele cha kulipwa laki mbili na elfu hamsini kila Simba itakapopata ushindi.
Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuvaa jezi Nyekundu na Nyeupe mali ya Wekundu wa Msimbazi.
Tayari Simba imefikisha jumla ya wachezaji wanne wapya ambao wanatarajiwa kuanza kuvaa jezi ya Simba wengine ni Jamal Mnyate na Peter Simwanza toka katika kikosi cha Mwadui

No comments