LIVERPOOL YAKARIBIA KUMSAJILI KIUNGO WA UBELGIJI

 Mazungumzo yanaendelea kati ya Liverpool na wakala wa kiungo kinda wa Ubelgiji na klabu ya Anderlecht  Samuel Bastien.


Livepool imepania kumsajili kijana huyo mwenye miaka 19 kwa dau la paundi milioni 4 na wakala wake Franklin Mala Makani ndiye anayehaha kufanikisha dili hilo.

Samuel alikua kwa mkopo katika klabu ya Avelino inayoshiriki ligi ya Serie B nchini Italia klabu ambayo ilipewa kipengele cha kumsajili moja kwa moja kama itamhitaji.

Mchezaji huyo ambaye huichezea timu ya taifa ya Ubelgiji chini ya miaka 21 yuko katika mapumziko mjini Marbella Spain na tayari Liverpool walishaanza mazungumzo nae mwezi March.


No comments

Powered by Blogger.