DI MATEO KOCHA MPYA WA ASTON VILLA

Klabu ya Aston Villa ya England inatarajia kumtangaza shujaa wa zamani wa Chelsea Roberto Di Mateo kama kocha wao mkuu.


Aston Villa iliyoshuka daraja msimu huu uliomalizika katika ligi kuu ya England imepania kurudi katika ligi hiyo kwanza kwa kumpata kocha makini huku majina mengi yakitajwa kabla likiwemo la David Moyes,Nigel Peason na Sean Dyche

Mmiliki wa klabu tajiri wa Kichina Tony Xia ameonekana kumkubali mno Di Mateo na mazungumzo ya mwisho yanaendelea na Tangazo rasmi litatolewa na klabu hiyo muda wowote.

Di Mateo ameshinda ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2012 akiwa na Chelsea kabla ya kutimuliwa na badae kujiunga na Schalke 04.

No comments

Powered by Blogger.