CHELSEA WAMBANIA BEKI WAKE KUBAKI MOJA KWA MOJA UJERUMANI
Klabu ya Chelsea imesema haina mpango wa kumuuza beki wake chipukizi Andreas Christensen kwa Borussia Monchengladbach ya Ujerumani ambao wameonekana kumtaka beki huyo.
Andreas mwenye miaka 20 anayecheza kama beki wa kati yuko katika msimu wake wa kwanza katika mkopo wa miaka miwili ambao Chelsea waliufanya kwa klabu hiyo ya Bundesliga.
Amekua na msimu mzuri sana akiwa na klabu hiyo hatua iliyopelekea mashabiki kumpigia kura ya kuwa mchezaji bora wa msimu wa klabu hiyo akimwacha Granit Xhaka aliyesajiliwa na Arsenal.
Monchengladbach wamepanga kuwapa Chelsea paundi milioni 18 na kama diki hilo likifanikiwa basi atakua amevunja rekodi ya klabu katika uhamisho ambayo ni paundi milion 11.5.
Chelsea wanamuona Christensen kama mbadala wa John Terry katika nafasi ya Ulinzi huku kocha Mpya Antonio Conte akitaka kusajili beki mmoja wa kati.

No comments