HII NDIYO SABABU ILIYOMFANYA MATTS HUMMELS KUIKATAA MAN UNITED

Swali ambalo mashabiki wengi wa  Manchester United bado wanajiuliza ni kwanini Timu yao ilishindwa kumsajili beki wa kinataifa wa Ujerumani Mats Hummels.



Imefahamika leo kwamba halikua swala la pesa lililopelekea Man United kushindwa kumsajili mchezaji huyo anayeimudu vyema nafasi ya beki wa kati kutoka katika klabu ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani.

Mats Hummels amesema leo alishakua tayari kujiunga na Manchester United badala ya Bayern Munich kama tu Man United wangeweza kufuzu kucheza katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Hummels mwenye miaka 27 alikua akihusishwa kujiunga na Manchester United kwa miaka kadhaa lakini ameamua kujiunga hivi karibuni na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich kutokana na United kukosa nafasi ya kucheza katika ligi ya mabingwa.

Wachezaji wengi barani Ulaya wana ndoto ya kucheza katika klabu inayoshiriki ligi ya mabingwa na imekua rahisi katika usajili kwa vilabu ambavyo hushiriki katika michuano hiyo na United yenyewe baada ya kushindwa kupata nafasi hiyo sasa itashiriki katika michuano ya Europa League wakiwa na kocha Jose Mourinho.


No comments

Powered by Blogger.