BAADA YA KUPATA KIUNGO SASA PEP GUADIOLA AMSAJILI MSHAMBULIAJI WA SPAIN

Baada ya kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Ilkay Gundogan, Kocha mkuu wa Manchester City amegeukia idara ya ushambuliaji.


Kocha Pep Guadiola ameamua kumsajili Mshambuliaji wa kumataifa wa Spain na klabu ya Celta Vigo Manuel Agudo Duran maarufu kama Nolito

Nolito ambaye yuko na timu yake ya taifa katika michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa alikua akihusishwa kwa kiwango kikubwa kurejea katika kikosi cha Barcelona.

Ikumbukwe mchezaji huyu alipewa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Barcelona mwaka 2010 na kocha Pep Guadiola wakati huo akiifundisha Barcelona.

 Nolito anajiunga na Manchester City kwa ada ya Uhamisho wa paundi miloni 14.1 kutoka Celta Vigo akiwa na umri wa miaka 29 hivi sasa.

Nolito alikua akihusishwa na kujiunga na Arsenal pia na alikua amefunga bao 39 katika mechi 100 za ligi akiwa na Celta Vigo tangu alipojiunga na Timu hiyo akitokea Benfica mwezi Julai 2013.


No comments

Powered by Blogger.