ARSENAL KUKAMILISHA UHAMISHO WA JAMIE VARDY LEO

Baadaya kutoka taarifa za kushtukiza wiki hii kuhusu Nia ya Arsenal kutaka kumsajili mshambuliaji wa England anayekipiga Leicester City basi dili hilo linaweza kukamilika leo.


Vardy anatarajiwa kwenda London kukamilisha vipimo vya afya tayari kutangazwa kuwa mchezaji wa Arsenal.

Kiasi cha paundi milioni 20 kimetajwa kama dau linaloweza kumng'oa mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 24 katika ligi msimu uliopita na kuiwezesha Leicester City kutwaa ubingwa na mshahara wa paundi 80,000 kwa wiki.

Bado habari za usajili wa Vardy hazijathibitishwa rasmi na Arsenal hata Leicester City na Wapenda soka wengi wanasubiri kuona kama Vardy mwenye miaka 29 atamwaga wino leo.

No comments

Powered by Blogger.