MOHAMED SALAH AIPELEKA MISRI KATIKA AFCON MWAKANI

Mabingwa mara 7 wa kombe la mataifa ya Afrika Mafarao wa Misri wameweza kutinga katika fainali zijazo za kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuwalaza wenyeji Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa bao 2-0.


Uzoefu wa wachezaji wa Misri ulikua ndiyo silaha tosha ya ushindi wao kwani licha ya Taifa Stars kumiliki mpira kwa muda mrefu ilishindwa kabisa kupata bao.

Mshambuliaji wa Misri anayeichezea AS Roma Mohamed Salah ndiye aliyekua shujaa kwa kufunga mabao yote mawili katika mchezo huo ambao nahodha wa Stars Mbwana Samata alikosa penati.

Kwa matokeo hayo Misri inatinga katika fainali zijazo za kombe la mataifa ya Afrika zitakazopigwa nchini Gabon.

No comments

Powered by Blogger.