COPA AMERICA : BRAZIL YAANZA KWA SARE, PERU YAPATA USHINDI NA KUONGOZA KUNDI B

Michuano ya Copa America imeingia katika siku yake ya pili usiku wa kuamkia leo kwa michezo mitatu kupigwa.


Michuano hiyo inayofanyika nchini Marekani imeshuhudia wababe wa dunia Brazil wakilazimishwa sare ya bila kufungana na Ecuador katika mechi ya pili yakufungana

Katika mechi ya awali ya kundi hilo B Peru waliifunga Haiti kwa bao 1-0 katika mchezo ambao Haiti ilionyesha soka safi na kuibana Peru.

Shujaa wa mechi hiyo alikua ni mshambuliaji wa Peru anayeichezea Flamengo ya Brazil Jose Paulo Guerrero.

Katika mechi nyingine ilishuhudiwa sare ya bila kufungana kati ya Costa Rica na Paraguay katika kundi A.

Michuano hiyo itaingia siku yake ya 3 usiku wa leo kwa saa za Afrika mashariki ambapo mechi zitakua kama ifuatavyo


  • Jamaica vs Venezuela (saa 6 Usiku)
  • Mexico vs Uruguay (saa 9 usiku)


No comments

Powered by Blogger.