MASHARTI YA HIGUAIN KUJIUNGA NA CHELSEA HUENDA YAKAMKIMBIZA DIEGO COSTA

Mshambuliaji  Gonzalo Higuain amesema yuko tayari kujiunga na Chelsea kwaajili ya msimu ujao wa ligi lakini akiwapa masharti Chelsea.


Dili la usajili wa mshambuliaji huyo wa Napoli litaigharimu Chelsea kiasi cha paundi milioni 42 lakini sharti kubwa alilowapa ni kutotaka kucheza kama mshambuliaji chaguo la pili nyuma ya Diego Costa.

Tayari Diego Costa ameshajihakikishia namba katika kikosi cha Chelsea akiwaacha washambuliaji wengine Loic Remy na Radamel Falcao ambao hupata nafasi tu pale ambapo Costa anakosekana.

Tayari kocha mpya wa Chelsea Antonio Conte ameshaiambia bodi ya Chelsea kwamba Higuain ni mmoja kati ya wachezaji anaofikiria kuwaleta pale darajani na Mchezaji mwenyewe anaonekana kukubali kujiunga na Chelsea hata kama haitacheza ligi ya mabingwa msimu ujao.

Kama Chelsea watakubaliana na matakwa ya mchezaji huyo na kumsajili ina maana Diego Costa kama atabaki basi lazima akubali kusugua benchi.

UFANANISHO

GONZALO HIGUAIN

miaka: 28
Michezo aliyocheza: 425
Magoli aliyofunga : 217
Pasi za magoli (assists ) : 82

DIEGO COSTA

miaka: 27
Michezo aliyocheza: 349
Magoli aliyofunga : 139
Pasi za magoli (assists ) : 50




No comments

Powered by Blogger.