RONALDO YUKO KAMILI KUIVAA MAN CITY, BENZEMA AKOSEKANA

Baada ya kukosekana katika mechi zilizopita za nusu fainali ya klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Manchester City na ile ya ligi kuu Spain dhidi ya Real Sociedad Cristiano Ronaldo leo atarudi dimbani.


Akiwa mwenye furaha katika mazoezi ya timu yake ya Real Madrid ambayo leo itahitaji ushindi pekee kuweza kutinga hatua ya fainali itakayochezwa Tarehe 20 Mwezi huu kule Milan Italia.

Ronaldo ambaye mchango wake katika Real Madrid msimu huu ndiyo ulioiwezesha timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali licha ya kufungwa katika mechi ya awali dhidi ya Wolfsburg.

Katika magoli 26 waliyofunga Real Madrid msimu huu katika michuano hiyo mikubwa kabisa katika ngazi ya klabu Ronaldo ameshiriki katika magoli 20 akifunga magoli 16 na kutoa pasi za magoli 4.

Pigot kubwa kwa Real Madrid leo litakua kukosekana kwa mshambuliaji wake Karim Benzema ambaye anaugulia maumivu ya goti.

Tumekuwekea hapa picha za mazoezi ya Real Madrid kuelekea katika pambano lao la leo dhidi ya Manchester City katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid.








No comments

Powered by Blogger.