HATIMAYE: LUCA TONI ATANGAZA KUSTAAFU KUCHEZA SOKA

Aliyekua mshambuliaji wa kimataifa wa Italia na klabu ya Verona Luca Toni ametangaza kustaafu kucheza soka.


Toni amesema ameamua kwa hilarious yake kustaafu kucheza soka baada ya mechi ya nyumbani dhidi ya wa ajili wake wa zamani Juventus Jumapili ya mwisho wa wiki hii.

Toni katika maisha yake ya soka amevichezea  vilabu kadhaa kwa mafanikio makubwa ikiwemo Juventus na Bayern Munich lakini pia ni mmoja kati ya wachezaji wa kikosi cha  Timu ya taifa ya Italia kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 2006.

Katika Serie A Toni ameshavichezea vilabu 8 akifunga magoli 156 katika mechi 343 za Serie A.

Anakumbukwa zaidi msimu uliopita alipoweka rekodi ya kipekee kwa kuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa katika historia ya ligi kuu ya Italia akiwa na umri wa miaka 38 kuwa mfungaji bora akifunga mabao 22 sawa na Mauro Icardi

Toni alipokuwa Ujerumani aliweza pia kuchukua tuzo ya mfungaji bora wa huko msimu wa mwaka 2007/2008.


No comments

Powered by Blogger.