HIZI NDIZO JEZI MPYA ZA CHELSEA MSIMU UJAO
Klabu ya Chelsea leo imezindua jezi mpya zitakazotumiwa na timu hiyo katika mechi zao za nyumbani msimu ujao.
Jezi hizo ambazo zimetengenezwa na kampuni ya Adidas zina mwonekano wa tofauti kidogo na jezi za sasa za timu hiyo tofauti kubwa ikionekana katika kola ya jezi hizi mpya ambazo zina alama ya "V" tofauti na zile za awali ambazo zilivaliwa katika mechi ya mwisho Juzi dhidi ya Tottenham Hotspurs
Mwonekano wa mbele wa jezi hizo mpya za Chelsea bado unatawaliwa na wadhamini wakuu wa timu hiyo kampuni ya matairi ya Yokohama katika mkataba wao wa paundi milioni 200 waliosafiri mwanzoni mwa msimu huu.
Jezi hizo zitaonekana kwa mara ya kwanza zilivaliwa na Chelsea katika mechi ya mwisho kabisa katika ligi kuu msimu huu dhidi ya mabingwa wapya Leicester City katika dimba la Stamford Bridge.
No comments