SAFARI YA WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA NCHINI SUDAN SASA YAOTA MBAWA

Matumaini ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba kushiriki michuano ya NILE BASIN nchini Sudan imeota mbawa baada ya Taarifa kutoka leo kwamba michuano hiyo imeahirishwa.
Tumekuwekea hapa Taarifa kamili kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania TFF.



Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeahirisha michuano ya kuwania Kombe la nchi unakopita Mto Nile ‘Nile Basin Cup’.

Taarifa iliyotumwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye inasema kwamba wamepata taarifa za kuahirisha michuano hiyo kutoka kwa waratibu wakiwamo wenyeji Sudan.

Taarifa imesema wamekubaliana kuahirisha mpaka hapo watakapotangaza tena hivyo Simba iliyoteuliwa na TFF kushiriki michuano hiyo, imetaarifiwa kusubiri tarehe mpya ya mashindano.

No comments

Powered by Blogger.