AZAM PUMZI IMEKATA : YATOKA SARE NA JKT RUVU CHAMAZI, NDOTO ZA UBINGWA NDO BASI TENA
Ni kama wamepata Pumzi vile, ndivyo kwa haraka unaweza kusema kufuatia kusuasua kwa mabingwa wa kombe la Kagame Azam FC katika mechi zao za mwisho katika ligi kuu Tanzania bara.
Ikiwa katika dimba lake la nyumbani pale Azam Complex Chamazi Azam FC ilishindwa kulinda mabao mawili waliyotangulia kufunga kipindi cha kwanza dhidi ya JKT Ruvu na mchezo huo kumalizika kwa Sare ya bao 2-2.
Mapacha Kipre Tchetche na Kipre Balou walijitahidi kuiweka mbele Azam FC mpaka mapumziko kwa mabao waliyofunga lakini kipindi cha pili safu ya ulinzi ya Azam ikawaruhusu JKT Ruvu wanaonolewa na Abdallah Kibadeni kusawazisha mabao hayo kupitia kwa Saad Kipanga na Najim Maguli.
Kwa Sare hiyo ni dhahiri sasa mbio za ubingwa zimefika ukingoni kwani hata ikishinda mechi zote tatu zilizobaki itafikisha pointi 79 wakati Yanga wanaoongoza wana pointi 78 wakiwa na michezo mitatu pia mkononi.
No comments