YAMETIMIA: FAINALI MABINGWA ULAYA NI REAL MADRID VS ATLETICO MADRID, MAN CITY YATUPWA NJE
Mabingwa mara 10 wa Michuano ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya Real Madrid wametinga katika fainali ya michuano hiyo kwa mara nyingine msimu huu baada ya kuitupa nje Manchester City toka England.
Real Madrid imeitandika Manchester City kwa bao 1-0 katika mechi ya marudiano ya nusu fainali ya michuano hiyo mechi iliyopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Manchester City Waliokua wakihitaji Sare tu kutinga fainali walijikuta wakishindwa kabisa kuikabili kasi ya Real Madrid na kupelekea kujifunga bao pekee katika mchezo huo baada ya Fernando kujifunga katika harakati za kuokoa shuti la Gareth Bale
Kwa matokeo hayo Real Madrid watakutana tena na Atletico Madrid katika fainali ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya katika dimba la San Ciro jijini Milan Italia ikiwa ni marudiano ya fainali ya michuano hiyo msimu wa mwaka 2013/2014 wakati Real Madrid waliponyakua taji lao la 10.
Hii ni mara ya 14 kwa Real Madrid kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo ikiwa ni rekodi ya kipekee na katika mara zote hizo walizotinga fainali wamepoteza mara 3 tu.
Kama hukuangalia mechi hiyo unaweza kuangalia highlights hapa

No comments