JUAN MATA AIBEBA MAN UNITED KUIBUKA NA USHINDI UGENINI

Akicheza katika namba anayoipenda uwanjani yani namba 10 kiungo Wa Kihispania Juan Mata Leo alifunga bao pekee katika mchezo muhimu kwa Man United walipoifunga Norwich bao 1-0.



Mchezo huo Wa ligi kuu nchini England ulipigwa katika dimba la Carow Road jijini Norwich ambapo Man United walipata bao hilo pekee kipindi cha pili baada ya juhudi za Wayne Rooney kutumia makosa ya mlinzi Wa Norwich Sebastian Bassong na kumpasia Mata as liyefunga kiulaini.

Kwa matokeo hayo Man United wanafikisha pointi 63 katika nafasi ya tano huku Norwich wakibaki na pointi zao 31 katika nafasi ya 19.


No comments

Powered by Blogger.