BILIONEA SHABIKI WA MAN UNITED AJITOKEZA KUINUNUA CHELSEA, ABRAMOVICH AGOMA
Mmiliki wa Klabu ya Chelsea Roman Abramovic amekataa ofa ya kuiuza Klabu hiyo ofa iliyotolewa na Tajiri Mwingereza ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu ya Manchester United Jim Ratcliffe.
Bilionea huyo alijitokeza kutaka kuinunua Chelsea wakati huu ambapo Abramovic akikumbwa na matatizo katika hati yake ya uhamiaji nchini England na kupelekea kusitisha upanuzi wa uwanja wa Stamford Bridge.
Ni mwaka wa 15 sasa Abramovic anaimiliki Chelsea na taarifa toka Ndani ya klabu hiyo zinasema sio tu ofa ya Jim iliyokataliwa Bali zipo oaf nyingine toka China ambazo zilitaka kuinunua Chelsea.
Jim Ratcliffe mfanyabiashara mwenye utajiri Mara mbili ya alionao Abramovic anamiliki pia timu katika ligi ya Uswisi na ni shabiki mkubwa wa Manchester United lakini Mara nyingi amekuwa akiangalia mechi za Chelsea kutokana na ukaribu wake na mahali anapoishi jijini London.
Thamani ya Chelsea inakaridiriwa kuwa paundi Bilioni 1 huku utajiri wa Jim Ratcliffe ni Paundi Bilioni 21.05.
No comments