TFF YAWAPA YANGA MPAKA JUMAPILI KUJITATHMINI KUJITOA KAGAME CUP.

Shirikisho la Soka nchini Tanzania T.F.F limewapa viongozi wa Yanga mpaka Jumapili hii kuweza kujitathmini kuhusu barua yao waliyoandika kutaka kujitoa katika mashindano ya Kombe la Kagame.

Rais wa Shirikisho Hilo Bwana Wallace Karia amesema sababu walizotoa Yanga hazina mashiko kwani hata timu nyingine shiriki zina Ratiba ngumu pia mfano ni Gor Mahia ya Kenya ambayo inashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika tena wakiwa Kundi moja na Yanga na bado wanashiriki mashindano ya SportPesa Super Cup ambayo fainali yake ni kesho.

Yanga waliiandikia barua TFF ya kujitoa kushiriki kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati yanayotarajiwa kuanza mwishoni wma mwezi huu Kwa madai kwamba wamebanwa sana na Ratiba wakiwa wamepangwa Kundi  A pamoja na Simba, St. George ya Ethiopia na  Dakadaha ya Somalia.

No comments

Powered by Blogger.