SIMBA KUMKOSA HARUNA NIYONZIMA KESHO DHIDI YA GOR MAHIA
Wekundu wa Msimbazi Simba ambao ni Mabingwa wa Soka nchini Tanzania kesho Jumapili wataingia uwanjani kuwania ubingwa wa Sportpesa Super Cup dhidi ya Mabingwa wa Kenya Gor Mahia bila ya Kiungo wao Haruna Niyonzima.
Haruna atakosa mchezo wa kesho kufuatia kadi mbili za njano alizopata katika mechi zilizopita hivyo kumfanya kukosa mchezo huo muhimu Kwa Simba.
BINGWA wa michuano hiyo sambamba na kuondoka na Kombe na kitita cha fedha lakini pia atapata nafasi ya kwenda jijini Liverpool England kucheza mechi ya Kirafiki dhidi ya Everton ya huko.
No comments