KOMBE LA DUNIA, ARGENTINA YAPATA PIGO, LANZINI AUMIA

Ikiwa imebaki wiki moja kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la dunia Kiungo wa kimatifa wa Argentina anayeichezea West Ham United Manuel Lanzini ameondolowa kwenye orodha ya wachezaji watakaoiwakilisha Argentina katika fainali hizo zitakazochezwa nchini Russia.

Lanzini ameondolewa baada ya kuumia Mazoeni leo asubuhi wakati wa maandalizi ya mwisho kabla ya kusafiri kwenda Russia kufuatia kufutwa kwa mechi yao ya kirafiki Jumamosi dhidi ya Isarael jijini Jerusalem kwaajili ya usalama.

Lanzini mwenye umri wa miaka 25, ameichezea timu ya Taifa ya Argentina michezo minne tu na fainali hizi za Kombe la Dunia yeye ni mmoja kati ya nyota waliotarajiwa kufanya makubwa.

No comments

Powered by Blogger.