HARRY KANE AJIFUNGA SPURS MPAKA 2024.

Nahodha wa Timu ya taifa ya England Harry Kane ameamua kusaini mkataba mpya wa miaka sita kuichezea Tottenham Hotspurs mkataba utakaomweka White Hart Lane hadi mwaka 2024.

Mshambuliaji Huyo mwenye miaka 24, ameweza kuifungia timu yake mabao 30 katika ligi kuu ya England msimu uliomalizika Hivi karibuni na Ku saidia Spurs kumaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City na Manchester United.

 Kane anatarijiwa kuiongoza Timu yake ya Taifa ya England katika mashindano ya kombe la dunia yanayotegemewa kuanza nchini Urusi wiki ijayo.

Kane ndiye mfungaji bora wa Tottenham akiwa  ameishaichezea mechi 150 na kuifungia magoli 108.

Sambamba na mkataba huo Harry Kane amepata nyongeza ya msahara atakaolipwa mpaka kufikia paundi 200,000 kwa wiki ikiwa ni mara mbili ya mshahara anaopokea hivi sasa.

Taarifa za Kane kuongeza mkataba wake wa kyitumikia Spurs ni faraja nyingine wanayopata mashabiki wa timu hiyo baada ya Mwezi Uliopita Kocha wa timu hiyo Mauricio Pochettini nae kusaini mkataba mnono wa miaka mitano japo kuna shinikizo kubwa kwa Real Madrid wanaoonekana wanahitaji huduma yake.

No comments

Powered by Blogger.