KAPOMBE AFURAHIA KUKUTANA NA GOR MAHIA
Nyota wa timu ya Simba, Shomari Kapombe amefurahia kukutana na timu ya Gor Mahia katika mchezo wa fainali wa michuano ya SportPesa Super Cup.
Kapombe amesema Gor ni timu bora kwenye mashindano hayo ambapo wanaamini watapata upinzani mkubwa kutoka kwa mabingwa hao wa Kenya.
Kiraka huyo ameongeza kuwa mchezaji anatakiwa kukutana timu bora ili kuimarisha kiwango chake kwahiyo kukutana na Gor imekuwa jambo zuri.
"Binafsi nimefurahi kukutana na Gor kwakua ni timu bora kwahiyo mechi ya fainali itakuwa ya upinzani mkubwa na mimi kama mchezaji napenda mechi zenye upinzani mkubwa," alisema Kapombe.
Kapombe amekuwa kwenye kiwango bora tangu aliporejea kutoka majeruhi yaliyo muweka nje ya uwanja kwa muda mrefu na kuingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza.
Mechi ya fainali kati ya Simba dhidi ya Gor Mahia itafanyika katika uwanja wa Afraha kuanzia saa 9 alasiri.

No comments