LEICESTER CITY YAMNASA JOHN EVANS

Mabingwa wa ligi kuu Soka nchini England mwaka 2015/2016 klabu ya Leicester City imekamilisha uhamisho wa mlinzi wa zamani wa klabu ya Manchester United na West Brom John Evans.

Evans anajiunga na Leicester City kwa mkataba wa miaka mitatu na atakua akilipwa kiasi cha paundi 80,000 na imewagharimu kiasi cha paundi milioni 3 pekee Leicester City kumnyakua beki huyo anayemudu vyema nafasi ya beki wa Kati na beki wa pembeni.

Mkataba wa John Evans na klabu yake ya West Brom ulitaja kiasi cha paundi milioni 3 Kwa yeye kuhama klabu hiyo iwapo itashuka daraja na ndicho kilichofanywa na Leicester kumpata mchezaji huyo ambaye awali West Brom waligoma kumwachia Kwa paundi milioni 20.

No comments

Powered by Blogger.