BARANSANANIKIYE ATIKISA VILABU KATIKA USAJILI NCHINI BURUNDI



Na  Niyikuza Sarara Yves : Burundi

Mwaka 1995 Ndiyo mwaka aliozaliwa mshambuliaji Jackson Baransananikiye ambaye anatikisa sasa katika usajili  katika timu zinazoshiriki ligi kuu ya hapa Burundi maarufu kama Primus League huku vigogo Vinne vikimwania mchezaji Huyu machachari aliyezaliwa jijini Bujumbura kutaka kumsajili.

Tayari k. labu ya Vital'O FC kupitia Kwa kocha wake mkuu Kanyankore Gilbert Yaounde imeshaweka bayana nia yake madhubuti ya kutaka kumsajili kuichezea klabu hiyo katika ligi na michuano mingine.

Ukiacha Vital'O Timu ya Musongati FC ya mkoani Gitega nayo inamsaka mchezaji huyo na tayari mazungumzo kati ya timu hiyo na mchezaji huyo yameanza lakini pia zipo timu za Ngozi City na Black Eagle ambazo nazo zimeweka wazi kumuhitaji.

Jackson Baransananikiye amekua mfungaji bora wa michuano ya Copa Coca Cola hapa Burundi na kupata zawadi ya kwenda nchini Afrika Kusini kwaajili ya mazoezi lakini pia ameibuka katika nafasi ya tatu Kati ya wafungaji bora wa ligi kuu ya hapa Kwa mwaka 2017/2018.

 Ikumbukwe mwaka 2016/2017 Jackson alipata nafasi ya kucheza Soka la kulipwa nchini Djibouti katika klabu ya Dikhil FC ambapo alifunga mabao 12 kabla ya kurejea Burundi na kujifunga na Flambeau de d'est na kufanikiwa kufunga mabao 7 msimu ulioisha na kufanya klabu hiyo kutaka kuendelea kuwa nae na tayari imeomba kufanya nae mazungumzo.

No comments

Powered by Blogger.