RASMI: YANGA YAIKIMBIA SIMBA KAGAME, YATANGAZA KUJITOA

Kitimtim cha michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki kilichopangwa kutimua vumbi hapa Tanzania kuanzia Juni 28 hadi Julai 13 jijini Dar es Salaam huenda kikakosa msisimko uliotarajiwa baada ya habari ambazo tumezithibitisha  kusema kuwa moja kati ya vigogo wa soka katika ukanda huu, Yanga ya Tanzania wameomba kujitoa katika michuano hiyo.

Sababu waliyoitoa Yanga ni kubanwa na ratiba kutokana na na kushiriki katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ambapo wanataraji kucheza na Gor Mahia mnamo Julai 18 jijini Nairobi.

Akiongea na mtandao huu, Godlisten Chicharito kutoka idara ya habari ya Yanga amesema "Ni kweli, Yanga imejitoa Kagame kwa sababu ratiba ya shirikisho inatubana"

Taarifa tulizonazo ni kwamba baada ya kutolewa katika michuano ya Sport Pesa Super Cup huko Nakuru, wachezaji wa Yanga wamepewa mapumziko hadi Juni 25.

Yanga walipangwa katika kundi C pamoja na watani wao Simba, Dakadaha kutoka Somalia pamoja na St. George kutoka Ethiopia.

Tayari Mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu Tanzania bara wamewasilisha barua ya kujitoa kwa shirikisho la soka nchini TFF na lile la Afrika Mashariki na kati yani CECAFA

No comments

Powered by Blogger.