KERR HAICHUKULII POA SIMBA
Kocha mkuu wa timu ya Gor Mahia, Dylan Kerr amebainisha kuwa watapata upinzani mkubwa kutoka kwa Simba kwakua wanazidi kuimarika kila mchezo.
Gor itakutana na Simba katika mchezo wa fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup siku ya Jumapili katika mchezo ambao Kerr anaamini utakuwa mgumu.
Muingereza huyo ambaye aliwahi kuinoa Simba amesema Wekundu hao wanazidi kuimarika kila siku kitu kinachofanya mchezo huo kuwa mgumu.
"Simba ni timu nzuri ina wachezaji wengi vijana ambao wana kasi kubwa, nategemea mchezo utakuwa mgumu ingawa nakiamini zaidi kikosi changu," alisema Kerr.
Gor ndio timu iliyofunga mabao mengi katika michuano hiyo ikicheka na nyavu mara tano ikiwa haijafungwa wakati Simba ikiwa haina bao hata moja lakini nayo haijaruhusu bao.
Mchezo wa fainali ya michuano hiyo utapigwa siku ya Jumapili saa 9 alasiri ukitanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu Kati ya Kakamega Homeboyz dhidi ya Singida United.

No comments