REAL MADRID YAMWEKA "SOKONI" RONALDO

Taarifa kutoka Nchini Spain kupitia chanzo cha habari Mundo Deportivo zinaeleza kwamba Real Madrid wameweka wazi dau la Euro milioni 200 kwa timu yoyote itakayohitaji huduma ya mchezaji bora wa dunia na Mshambuliaji wa timu hiyo Cristiano Ronaldo.

Mwanzoni ilikua ngumu kufikiria kumnunua Ronaldo kwakua mkataba wa mchezaji huyo unaoisha mwaka 2022 unaweza kwamba Ile timu iweze kumnunua Ronaldo itabidi itoe kiasi cha Euro Bilioni 1 ili kuvunja mkataba wa nyota huyo.

Tetesi za Ronaldo kuihama Real Madrid zilianza baada ya fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya ambapo Real Madrid waliibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Liverpool huku Ronaldo akizungumza  maneno ambayo yaliashiria anataka kuondoka Santiago Bernabeu.

"Imekua ni furaha yangu kuichezea Real Madrid ila nitaongea mengi katika siku zijazo" Alisema Ronaldo Mara baada ya kumalizika mchezo wa fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya.

No comments

Powered by Blogger.