DONALD NGOMA NJE TENA WIKI TISA

Imefahamika kwamba Mshambuliaji mpya wa Azam FC Donald Ngoma atakaa nje Kwa wiki Tisa kuanzia sasa Ili awe tayari kuitumikia klabu yake katika michuano mbalimbali

Akiongea na www.wapendasoka.com Daktari mkuu wa Azam FC Dr. Mwankemwa Mwanandi
Amesema uchunguzi wa vipimo mbalimbali vya afya alivyofanyiwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Zimbabwe akiwa nchini Afrika Kusini vilibaini kwamba Ngoma atatakiwa kukaa nje Kwa muda huo Ile aweze kupona kabisa tatizo linalomkabili.

Dr. Mwankemwa Mwanandi ametoa taarifa hiyo Ikiwa ni saa chache tangu watue nchini yeye na Donald Ngoma wakitokea Afrika Kusini ambako Azam FC waliamua kumpeleka kwaajili ya uchunguzi wa afya yake.

"Hakuna upasuaji atakaofanyiwa Donald ila atafanya tu mazoezi mepesi wakati huu wa wiki Tisa ili aether uwanjani" alisema Dr. Mwankemwa.


Azam FC ilimsajili Donald Ngoma toka Yanga huku akiwa hajacheza takribani msimu mzima wa ligi kuu Soka Tanzania bara kufuatia kuwa majeruhi.

No comments

Powered by Blogger.