CHELSEA YAENDELEA KUGAWA POINTI EPL, NEWCASTLE HALI MBAYA

Waliokua mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini England Chelsea wameendelea kugawa pointi msimu huu baada ya kukubali kichapo cha bao 3-2 toka kwa Sunderland.


Sunderland walio katika hatari ya kushuka Daraja walihitaji pointi 3 kutoka katika mchezo huo huku wakiombea Newcastle United ifungwe au kutoka Sare.

Sunderland wakafanikiwa kupata ushindi  na Newcastle wakatoa Sare ya bila kufungana  ugenini dhidi ya Aston Villa

Swansea City wakiwa nyumbani waliitandika West Ham  bao 4-1 huku Bournemouth wakienda Sare ya bao 1-1 na West Bromwich Albion huku Crystal Palace  wakiinyuka Stoke City bao 2-1.

No comments

Powered by Blogger.