RASHFORD ALIYEWAUA ARSENAL KAWAMALIZA MAN CITY KWAO

Nyota imezidi kung'ara kwa chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford baada ya kaibeba timu yake tena na safari hii ameiongoza United kutoa kichapo kwa majirani zao Manchester city.




Pambano hilo la Wapinzani wa jiji la Manchester likishuhudia Man United ikiibuka na ushindi wa bao hilo 1-0 bao pekee La dakika ya 16 ya kijana Marcus Rashford baada ya kumlamba chenga beki Martin Demicheles na kupiga mpira ukiomshinda kipa Joe Hart.

Ikumbukwe kuwa Rashford aliwatungua Arsenal pia bao 2 katika ushindi wa bao 3-2 walioupata Manchester United mwezi uliopita katika dimba la OLD Trafford.

Kama kawaida Wapenda Soka blog tumekuwekea highlights za mchezo huo kama hukupata muda wa kuangalia

MANCHESTER CITY 0-1 MANCHESTER UNITED



No comments

Powered by Blogger.