LIVERPOOL YAAAMBULIA KICHAPO KWA "WATAKATIFU" NEWCASTLE NA SUNDERLAND SARE

Licha ya kutangulia kupata mabao mawili Liverpool wamekumbana na kichapo cha bao 3-2 toka kwa Southampton ambao wanajulikana pia kama Watakatifu.



Pambano hilo la Ligi kuu ya England lilipigwa katika dimba La Saint Marys likishuhudia Liverpool walitangulia kupata bao 2 zilizofungwa na Philip Continho na Daniel Sturadge kabla ya Southampton kuzinduka na kupata mabao matatu kipindi cha pili Sadio Mane akifunga bao 2 na Graziano Pelle akifunga bao moja.

Katika mechi nyingine Newcastle ilitoshana nguvu na Sunderland kwa kufungana bao 1-1 Sunderland wakitangulia kufunga kupitia kwa Defoe lakini Mitrovic akaisawazishia Newcastle.

Kama hukuangalia mechi hizi mbili tumekuwekea hapa highlights unaweza kuangalia

SOUTHAMPTON 3-2 LIVERPOOL 



NEWCASTLE 1-1 SUNDERLAND 

No comments

Powered by Blogger.