TETESI ZA LEO ~ MAN UNITED WAAMBIWA WATOE PESA NDEFU KUMPATA LUKAKU, LIVERPOOL KUMUUZA STURRIDGE HUKU WAKIMTAKA CHICHARITO

Dirisha la usajili wa wachezaji katika ligi kuu za nchi mbalimbali linaendelea kushika kasi ambapo kutoka katika mitandao mbalimbali Tumekuandalia zile zitakazokufaa siku ya leo.



Kocha wa Manchester United Louis van Gaal mwenye miaka 64 anatarajia kuaondoka klabuni hapo baada ya kumalizika msimu huu ikiwa ni mwaka mmoja kabla hajamaliza mkataba wake pale Old Trafford (Daily Mirror)

Everton wameitaka Manchester United kutoa paundi milioni 65 kama kweli wanataka kumsajili mshambuliaji Raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku mwenye miaka 22.
(Sun)

Tottenham wamepeleka kiasi cha paundi milioni 23 kutaka kumsajili mahambuliaji wa Atletico Madrid Raia wa Colombia  mwenye miaka 29 Jackson Martinez. (Marca, via Daily Express)

West Ham wako mstari wa mbele kutaka kumsajili Mshambuliaji majeruhi wa Liverpool Daniel Sturridge mwenye miaka 26 na kiasi cha paundi milioni 18 kimeshatengwa kukamilisha dili hilo wakati huu ambapo kocha wa Liverpool Juggen Klopp anapanga kumuuza Sturidge.
(Brentwood Gazette)

Wakati huo huo Klopp anafikiria kumsajili mshambuliaji wa Bayer Leverkusen mwenye miaka 27 Javier Hernandez Chicharito ambaye kabla ya kujiunga na Leverkusen alitokea Manchester United
 (Calciomercato, via Metro)

Chelsea wanafatilia maendeleo ya mshambuliaji  wa Watford Odion Ighalo mwenye miaka 26 wakitaka kumsajili baada ya msimu huu wakati Radamel Falcao na Loic Remy wakionekana kutokua na nafasi kikosini na pengine wataruhusiwa kuondoka.
  (Daily Mirror)

AC Milan watatakiwa  kulipa kiasi cha paundi milioni 20 kama wanataka kumsajili kiungo wa Ubelgiji anayekipiga Katika klabu ya Manchester United  Marouane Fellaini.
 (Daily Express)

Mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino mwenye miaka 22 na winga wa Tottenham Andros Townsend mwenye miaka 24 wamebaki kuwa ndiyo machaguo ya kwanza kwa kocha Steve McLaren wa Newcastle United 24. (Newcastle Chronicle)

Dili la Kiungo wa Newcastle United Cheik Tiote kuhamia China katika klabu ya Shanghai Shenhua linatarajia kufa baada ya klabu hiyo ya China kutokua tayari kumlipa Tiote mwenye miaka 29 mshahara paundi 60,000 kwa wiki.
 (Guardian)

Kiungo wa Manchester City  Yaya Toure mwenye miaka 32, yuko tayari kusikia ofa ya klabu yoyote inayomtaka mwishoni mwa msimu huu.(Sun)

Liverpool wameanza mazungumzo na mabingwa wa Italia Juventus kutaka kumsaini mshambuliaji Alvaro Morata mwenye miaka 23 kwa paundi milioni 45  (Gazzetta World)  .

No comments

Powered by Blogger.